Monday , 7th Dec , 2015

Rapper Baghdad amesema kitendo cah kubadilisha muonekano wake ni moja ya sababu iliyompelekea ashuke kisanaa, tofauti na muonekano ambao alikuwa nao siku za nyuma.

Baghdad amefunguka hilo alipokuwa akiongea na timu ya Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa baada ya kubadilisha muonekano alikuwa na jukumu kubwa la kuaminisha watu kuwa Baghdad sio mnene tena kama ambavyo alikuwa zamani.

“Nadhani kwanza kubadilisha muonekano ndio sababu kubwa kibiashara kudrop, kwa sababu hata watu wa nje unapata show mkoani wakikutumia down payments, wakikutumia post unaona wanaweka picha ya zamani, sasa ukiangalia halisi sasa hivi uko model, wakiweka picha ya zamani mtaenda kugombana, kwa hiyo kulikuwa na nafasi kubwa sana ya kuzidi kuamisha watu kwamba Baghdad sio Bonge tena ni mwembamba”, alisema Baghdad.

Pamoja na hayo Baghdad ameongelea kazi zake alizozifanya hivi karibuni, na kusema kuwa kazi hizo likuwa ni kama kuwajulisha watu kuwa amerudi, lakini kazi ambayo amefanya na Roma ndio ambayo ameipa uzito na kisubiria.

“Kwangu mi nasema ngoma zilikuwa za utambulisho tu kwamba Baghdad amerudi na yuko model, ngoma ambayo tumefanya na Roma ndio project ambayo nadhani tunaitolea macho na wananchi nadhani wanaisubiri kwa hamu”, alisema Baghdad.