Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kilichomfanya Nahreel apagawe kwa Aika, hiki hapa

Wednesday , 15th Feb , 2017

Msanii na producer Nahreel amefunguka sababu kubwa iliyomfanya kumpenda mpenzi wake Aika, ambaye wanaunda naye kundi la Navy Kenzo kuwa ni kutokana na uzuri wa mashavu yake na siyo hips wala kifua kizuri.

Producer Nahreel akiwa na mpenzi wake Aika, kwa pamoja wanaunda kundi la Navy Kenzo.

Nahreel aliyasema hayo alipokuwa akiongea na EATV na kusema watu wengi wanadhani huenda alimpenda Aika kutokana na uzuri wake wa sura, uzuri wa umbo au uzuri wa kifua chake 

"Watu wengi wanadhani nimempenda Aika kutokana na umbo lake au kifua chake hapana, kikubwa kilichofanya nimepende Aika ni yale mashavu yake na nimekuwa namtania sana hata usiku napolala huwa nayapiga piga sana, hicho ndicho kilinifanya nimpende Aika" alisema Nahreel

Mbali na hilo Nahreel anasema katika miaka 9 ya mahusiano yao Aika amekuwa msaada mkubwa kwake kufikia lengo lake la kuwa producer mkubwa na kumiliki studio kubwa yenye viwango kwani alikuwa anampa moyo na kumsukuma kufika ndoto yake hiyo.

"Leo nasema huenda nisingekuwa na Aika labda nisingekuwa hapa leo, haya mafanikio niliyopata katika kila kitu katika miaka tisa toka nipo naye ni kutokana na msukumo wake hivyo naweza kusema haya mafanikio tumejenga kwa pamoja" alisisitiza Nahreel

Aika

Kwa upande wake Aika anasema katika mahusiano yao changamoto kubwa huwa wanaipata katika kufanya maamuzi hususani maamuzi ya mwisho katika kitu chochote.

"Siku zote katika mahusiano yetu tunapata changamoto kwenye final decision ya kitu chochote kile, hapo ndiyo huwa tunapishana au kunakuwa na ugumu zaidi kwetu, lakini katika miaka tisa toka nipo kwenye mahusiano na Nahreel sina cha kujutia kabisa kwani tuna mengi ya kujivunia katika maisha yetu na maisha ya mtu mmoja mmoja" alisema Aika 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya