Saturday , 20th Dec , 2014

Msanii wa miondoko ya rap, ROMA mkatoliki ameelezea kujivunia mafanikio yake kimuziki ambayo ni pamoja na kufunguka katika kuwagusa wananchi wa kawaida na kufikia hatua ya kupewa jina la 'Baba Paroko'.

ROMA

ROMA Mkatoliki, rapa ambaye sehemu kubwa ya muziki wake ameuelekeza kuzungumzia changamoto za kiuchumi kisiasa na kijamii za wananchi wa hali ya kawaida, amekuwa ni moja kati ya wasanii ambao wanajivunia kufunguka kwa muziki wao na kuwagusa wadau kutoka sekta mbalimbali ambao siku hadi siku wanazidi kuelewa umuhimu na nafasi ya sanaa ya muziki wa kizazi kipya.

Akizungumza juu ya hili, ROMA ametolea mfano wa yeye binafsi kuitwa na kiongozi wa dini ambaye amekuwa akimuelewa sana kazi zake kama ambavyo amekwishashuhudia kwa viongozi wengine wa kisiasa, na hapa anafafanua mwenyewe juu ya mchongo huu ambao unamuweka katika nafasi nyingine ya muhimu katika jamii, akiwa kama msanii wa Hip Hop.