Thursday , 1st Oct , 2015

Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania katika mashindano maarufu ya Televisheni ya Maisha ya Uhalisia Afrika na pia msanii wa muziki Julio Batalia, amesema kuwa amejipanga vizuri kujitambulisha rasmi katika gemu hiyo ya muziki mwezi Oktoba mwaka huu.

msanii wa muziki nchini Julio Batalia

Julio ambaye baada ya kuwekeza katika muziki kwa takriban miaka minne sasa, ameeleza kuwa, katika kipindi chote ambacho amekuwa akifanya muziki ikiwepo kushirikiana na mastaa wakubwa kama Chegge, Temba na wengineo, anaona dhahiri kuwa bado uwekezaji wake haujalipa, akiwa na uhakika wa kutokukosea safari hii kutokana na jinsi alivyojipanga.