Thursday , 20th Mar , 2014

Wasanii wakubwa wa muziki nchini Kenya, Jaguar pomoja na Juliani wamejitolea kumsaidia rapa mkongwe wa nchi hiyo, Johnny Vigetti ambaye ameripotiwa kusota katika shida kubwa ya uathirika wa dawa za kulevya.

Jaguar pamoja na Juliani wamesema kuwa, kinachofanyika sasa ni kujaribu kumtafuta msanii huyu kutokana na kutofahamu mahali alipo mpaka sasa, kwa ajili ya kumuingiza katika programu ya matibabu kuachana na dawa hizo.

Mastaa hawa wamesema kuwa, wameamua kujitolea kuchukua hatua hii kwa kutambua mchango na nafasi kubwa ya Johnny na kundi la Kalamashaka kama wasanii wenzao na pia kwa kutambua mchango wao katika harakati za awali za muziki wa Kenya.