GNL Zamba
Taarifa mpya kuhusiana na sakata hili zinaeleza kuwa, GNL amekwishapewa onyo na mdai wake ambaye amefahamika kwa jina Darius, kulipa pesa hizo kabla hajamchukulia hatua, ambapo sasa rapa huyu yupo katika jitihada za kuzichanga ili alipe deni hili.
GNL alichukua pesa hizi mapema mwezi wa pili, na kwa mujibu wa ripoti, baada ya onyesho lake la Aprili 18 kuzuiwa kufanyika, amekuwa na wakati mgumu kurudisha pesa za watu.