Thursday , 4th Sep , 2014

Msanii wa muziki DJ Cleo anatarajiwa kuandika historia ndani ya Afrika Mashariki, ambapo atatumbuiza katika siku maadhimisho ya miaka 25 ya Demokrasia ya nchi yake ya Afrika Kusini ndani ya Kenya.

msanii wa muziki wa nchini Afrika Kusini Dj Cleo

DJ Cleo atatoa burudani hii ndani ya jiji la Nairobi mwishoni mwa wiki, na atashirikiana na wasanii kama vile Anto Neo Soul kutoka Kenya, Dela pamoja na Vereso.

DJ Cleo amejijengea umaarufu mkubwa ndani ya Afrika mashariki kutokana na ngoma zake kali zenye maahadhi ya Kwaito.