Friday , 8th Feb , 2019

Msanii wa filamu bongo Diana Kimari, amefunguka juu ya tuhuma za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja na muigizaji mwenzake Wema Sepetu, hadi kufikia hatua ya kumchora mwilini mwake kwa tattoo.

Akizungumzia suala hilo, Diana amesema kwamba hajawahi kujihusisha jambo hilo na mtu yeyote ingawa anasikia tu, hivyo taarifa hizo hazina ukweli wowote, licha ya upendo mkubwa alionao kwa Wema Sepetu.

“Hicho kitu nimewahi kukisiskia, lakini sijawahi kue experience kinakuwa vipi, sijui kama kinaweza kufanyika, watu hawanielewi kwa sababu mimi siongei, siwezi kujibu, lakini nikimuongelea tu yule Da Wema sijui nimuweke vipi, nisimgharimu, kwa sababu hajawahi kuwa dada mbaya kwangu”, amesema Diana.

Diana ameendelea kuelezea kwamba, “naomba nimuombe msamaha, labda kwasababu nimechora tattoo yake inaweza ikamgharimu yeye, naomba anisamehe, naomba tu anisamehe, hii tattoo kweli mimi nimechora, ipo kwenye paja na siwezi kuifuta kwa sababu ni vitu vya kuchomana chomana, na nimemchora kwa upendo”.

Wawili hao kwa sasa wamepunguza ukaribu wao baada ya familia ya Wema Sepetu kumtaka kubadili aina ya marafiki alioano, na ndipo Diana alipoamua kuondoka nyumbani kwa Wema ambako inaaminika alikuwa amehamia na kuishi naye.