Friday , 24th Aug , 2018

Producer mkongwe wa bongo fleva, John Mahundi amefunguka na kumwagia mijisifa rapa King Crazy GK kuwa ni msanii mwenye jicho la pekee katika kutambua kipaji cha mtu pamoja na kuandika tungo zilizojaa hisia za ukweli nasio mtu wa ku-copy na ku-paste.

Mahundi ameeleza hayo alipokuwa anazungumza kwenye heshima ya bongo fleva iliyopo ndani ya kipindi cha PLANET BONGO kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema sio kwamba enzi walipokuwa wanafanya muziki hawakuwa watu wa kutunga mashairi kwa kuiba nchi za magharibi kama baadhi ya watu walivyokuwa wanafikiria, bali walijaliwa vipawa kwa kila mmoja wao ndani ya kundi la 'East Coast team'.

"Kitu ambacho tulikuwa tunafanya sisi ni kutengeneza muziki ambao tulikuwa na hisia nao, kwa mfano ukiangalia vitu vyote ambavyo alikuwa anazungumza King Crazy GK zilikuwa ni stori ambazo zimewatokea watu fulani 'either experience' navyo au watu wake wa karibu vimewatokea. kwa hiyo tulikuwa tunaongea ukweli kutoka moyoni sio kwamba tulikuwa tunakopi kutoka Marekani", amesema Mahundi.

Pamoja na hayo, Mahundi ameendelea kwa kusema "King Crazy GK alikuwa na jicho la kuona kipaji na alikuwa anafanya hivyo mara nyingi sikushangaa alipomleta Pauline Zongo kwenye 'Sister Sister".

Producer mkongwe John Mahundi.

Producer Mahundi ametengeza kazi nyingi kipindi cha miaka ya nyuma, ambapo hadi hii leo kuna baadhi ya nyimbo zikipigwa bado zina mashiko kwa wadau wa muziki. Mfano ulio hai ni wimbo wa 'Hii leo' wa msanii King Crazy GK ambao aliwashirikisha wakina AY na Mwana Fa.