Wednesday , 15th Oct , 2014

Uhasama kati ya wasanii Bebe Cool na Bobi Wine umeendelea kuchukua sura mpya kila siku, jipya katika hili ikiwa ni kauli ya Bobi Wine kusema kuwa hana tatizo lolote endapo Bebe atahitaji kutumbuiza katika maonesho yake.

Bobi Wine, Bebe Cool

Bobi Wine amekazia kuwa, kama hasimu wake huyu anaweza kusimama jukwaani na kuimba ngoma yake, basi pia anaweza kuhudhuria maonyesho yake anayoandaa ambayo ni maarufu zaidi.

Bebe Cool tayari amekwishajitetea kuwa, kitendo chake cha kuimba wimbo wa Bobi Wine jukwaani hivi karibuni ni kutokana na kulipwa kufanya hivyo, na si vinginevyo.