Barakah Da' Prince
Barakah, tofauti na wasanii wengine ambao huanza kufanya vizuri ndani ya mipaka ya nchi pekee, amesema nafasi hiyo imekuwa ni ya kipekee kwake hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa yeye ni moja kati ya mastaa wanaoipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya mipaka yake.
Star huyo pia ametaka mashabiki wake kufahamu mpango wake wa kuendeleza moto huo, akiwa anajitayarisha kwaajili ya kuachia rekodi mpya ambayo ni kolabo na msanii wa kike ambaye hakuwa tayari kumtaja, kazi ambayo itatoka rasmi mapema mwezi ujao.
Hapa unaweza kumsikiliza nyota huyu akifunguka zaidi mwenyewe;

