Monday , 18th May , 2015

Star wa muziki AY, akiwa na ukaribu mkubwa na msanii wa muziki Damian Soul kwa sasa kama kocha wa gemu ya star huyo anayepanda chati kwa kasi, amesema kuwa anajivunia kuweza kufanyakazi na msanii huyo.

wasanii wa miondoko ya bongofleva AY na mwanamuziki Damian Soul

AY ameweka wazi kuwa, Damian ambaye hivi karibuni wametokea kushiriki katika mashindano makubwa ya kusaka vipaji Afrika, yaliyofanyika nchini Kenya, amekuwa na nyota ya kipekee licha ya kutokushinda mashindano hayo, akiwa tayari anasakwa na mastaa wakubwa Afrika Mashariki, akiwepo Chameleone, Eric Wainaina na Rabbit kwaajili ya kolabo.