Thomas Tuchel kocha wa zamani wa Chelsea ya England amesaini mkataba wa miezi 18 kuiongoza timu ya taifa ya England. Kikosi hicho mabingwa wa kombe la Dunia mwaka 1966 kilikua chini ya Kocha wa muda Lee Carsley baada ya aliyekua Mkufunzi mkuu wa timu hiyo Gareth Southgate kujiuzulu mwezi Julai 2024. Tuchel anakuwa Mwalimu wa tatu ambaye si raia wa Uingereza kuiongoza England baada ya Sven- Goran Eriksson na Fabio Capello. Mjerumani huyo aliyewahi kushinda tuzo ya Kocha bora Ulaya na Dunia mwaka 2021 atasaidiwa na Antony Barry aliyefanya naye kazi Chelsea na Bayern Munich.
Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United ameujia juu Uongozi wa Manchester United baada ya Mabosi wa klabu hiyo kumuondoa Sir Alex Ferguson kwenye nafasi yake ya Ubalozi wa Mashetani Wekundu wa Jiji la Manchester. Ferguson Kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Mameneja wa Kingereza, aliiongoza Man U kushinda makombe 13 ya ligi kuu Uingereza, Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili na Kombe la klabu bingwa Dunia msimu wa 2007-2008. Cantona alikuwa Mchezaji muhimu alitoa mchango mkubwa kwenye klabu ya Manchester United alishinda makombe ya ligi EPL mara 4 katika miaka 5.
Picha ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere kulia na Steve Nyerere kushoto