Wednesday , 16th Oct , 2024

Geremiah Kwang (32) mkazi wa Kijiji cha Orkitikiti wilayani Kiteto mkoani Manyara amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Katika tuhuma hizo inadaiwa kuwa Geremiah alimuua mtoto huyo kwa kumpigiza chini mara kadhaa kisha kumsababishia majeraha mbalimbali sehemu ya mwili wake 

Akiwa mahakamani hapo Geremiah kabla ya kusomewa shitaka lake hilo alitakiwa asijibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya wilaya ya Kiteto Wilfred  Mollel mbele ya hakimu wa Mahakama Mosi Soro Sasy aliileza mahakama kuwa mtuhumuwa alitenda kosa hilo terehe 9/06/2024 katika Kijiji cha Orkitikiti Kata ya Lengatei

Amesema mtuhumiwa Geremiah amlitenda kosa kinyume na kifungu cha 196 ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2022.

Kwa kuwa mtuhumiwa hakutakiwa kujibu lolote Hakimu Sasy alieleza mahakamani hapo kuwa kesi hiyo inahamishiwa babati ambako  mtuhumiwa naye baada ya kuulizwa kama anataka usaidizi wa kisheria aliomba kupatiwa usaidizi huo na kukubaliwa.