Tuesday , 15th Oct , 2024

Msanii wa filamu Steve Nyerere 'Tivu Ake' amefunguka baada ya familia ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Charles Makongoro kumpiga stop kutumia jina la baba yao. 

Picha ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere kulia na Steve Nyerere kushoto

"Kunyamaza ni sifa ya Kukomaa, Matumizi Mazuri Mengine ya Mdomo ni kukaaa kimya sio kila jambo unajibu vingine vikupite kwa maslahi mapana ya heshima yako na watu waliokuzunguka.Nguvu ya kukaa kimya huwa Inatesa sana".

"Ukifikia hatua ya kuwa mtu mzima Mungu akakubariki hekima ya kunyamaza basi nyamaza kama mimi maana wanaokutazama nyuma ni wengi na wanao kutegemea ni wengi thamani yako Itakuwa kubwa kama Utaamua kunyamaza" ameandika Steve Nyerere