Waziri wa viwanda na biashara nchini Tanzania, Dkt Abdallah Kigoda.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara D. Abdalla Kigoda wakati akizungumza na wadau wa elimu wilayani Handeni kuhusu changamoto na mafanikio yatokanayo na elimu ili hatua za makusudi ziweze kufanywa kwa lengo la kukabiliana na vikwazo vinavyokwamisha jitihada za serikali za kukuza sekta ya elimu wilayani humo.
Kwa upande wake, Afisa Elimu wilayani Handeni Mgaza Mokiwa amesema wanafunzi zaidi ya watatu hadi wanne wanasongamana katika dawati moja huku wengine wakilala sakafuni wakati wanapoandika darasani hatua ambayo inachangia baadhi ya wanafunzi kushindwa kuandika kwa ufasaha.
Baadhi ya walimu waliozungumza kuhusu changamoto ya uhaba wa madawati katika shule zao wamesema tatizo hilo ni kubwa na limeanza kuchukua sura mpya kufuatia wanafunzi kulala kwenye udongo, hatua ambayo baadhi ya wazazi wamelalamikia tatizo kwa madai kuwa wanapata gharama kubwa ya kufua nguo za watoto wao kila siku.

