Thursday , 25th Jul , 2019

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni, amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, kuhakikisha ulinzi unaongezwa katika jengo jipya (Terminal 3) la uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Julius Nyerere.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni.

Akiongea leo Julai 25, 2019 alipotembelea eneo hilo, Masauni amesema ni wakati sasa vifaa vya kisasa vyenye uwezo wa kugundua bidhaa kama madini zinapopitishwa kinyemela zianze kutumika.

''Natoa maelekezo kwa IGP kuwa askari atakaowaleta hapa wawe wa kutosha na wenye sifa na uwezo wa kubaini bidhaa kama Madawa ya kulevya, Nyara za serikali na vitu vingine visivyopaswa kupita'', amesema.

Aidha ameeleza kuwa kwasababu kuna askari mbwa pia nao wanatakiwa kupelekwa wenye mafunzo stahiki, ili kuweza kuwatumia kubaini bidhaa zote ambazo hazitakiwi kupita bila uataratibu. 

Zaidi Tazama Video hapo chini