Tuesday , 8th Dec , 2015

Kesi ya upotevu wa shilingi bilioni 1 na milioni 75 inayowakabili waliokuwa watumishi wa shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO, Wilayani Karagwe mkoani Kagera na wafanyakazi wawili wa CHIKO imebadilishwa na kuwa ya uhujumu uchumi

Washtakiwa hao wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjini Bukoba ili waweze kuwasilisha ombi la dhamana na kurejeshwa tena rumande baada ya hakimu kuridhia ombi la mwendesha mashtaka wa serikali kutaka kesi hiyo kuwa ya uhujumu uchumi.

Akizungumza nje ya mahakama mwendesha mashtaka wa serikali Hashim Ng'wale alimuomba hakimu kubadili kesi kutoka na mazingira ya upelelezi na kiushahidi kesi hiyo ibadilike na kuwa ya kuhujumu uchumi.

Aidha washtakiwa hao walirejeshwa tena rumande kutokana na hakimu wa mahakama hiyo kudai kuwa mahakama yake haina uwezo wa kutoa dhamana kwa kesi za uhujumu uchumi.