Monday , 11th Jan , 2016

Raia 19 wa Burundi wakamatwa mkoani Mara kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria

Idara ya uhamiaji mkoa wa Mara imewakamata watu kumi na tisa raia wa nchini Burundi kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria kwa madai kuwa walikuwa wakitafuta hifadhi baada ya kukimbia ya kisiasa nchini mwao.

Ofisi ya uhamiaji mkoa wa Mara imesema kuwa wahamiaji hao haramu wamekamatwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari muda mfupi baada ya kuingia nchini na kwamba katika mahojiano wamedai kuwa wamefika hapa nchini ili kwenda katika kambi ya wakimbizi mkoani Kigoma.

Wakizungumza wakiwa chini ya ulinzi wa maafisa uhamiaji mkoani mara, wahamiaji hao haramu wamesema kuwa wamekimbia nchini mwao kutokana na machafuko ya kisiasa ambayo wamesema yamesababisha kukosekana na amani na vifo vya raia.