Friday , 19th Feb , 2016

Baraza la wanawake wa chama cha wananchi CUF limesema kuwa linakusudia kuitisha maandamano siku ya Jumatatu ili kusisitiza suala la amani nchini Zanzibar.

Makamu mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Severina Mwaijage, akihutubia katika mkutano wa hadhara

Akiongea leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa baraza hilo Severina Mwijage amesema kuwa kutokana na wanawake kuwa wahanga wa matukio mbalimbali nchini mara yanapotokea machafuko wao wanakusudia kufanya maandamano ili kufikisha ujumbe.

Aidha Mwijage amesema kuwa mpaka sasa hawaoni hali yeyote ya kuwepo kwa matumaini ya kupatikana kwa amani Zanzibar na badala yake wameendelea kuona amani ikitoweka kila kukicha

Mwenyekiti huyo ambe pia ni mbunge wa viti maalum amesema kuwa maandamano hayo yataanzia katika ofisi kuu ya CUF, Buguruni kuelekea ofisi ya makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu.

Aidha ameongeza kuwa wameshatoa taarifa kwa kamishna wa kanda maalumu ya Dar es salaam kamanda Simon Sirro na kumueleza njia zote watakazopita wakati wa maandamano hayo ambayo yataanzia asubuhi.