Friday , 17th Oct , 2014

Muungano wa asasi za kiraia katika masuala ya jinsia na Katiba nchini Tanzania umewashauri wananchi kuisoma na kuilewa katiba pendekezi kabla ya kutoa maoni yao ili kuwa na ufahamu wa kutosha wa kile kichomo ndani ya katiba hiyo.

Mwenyekiti wa Muungano wa asasi za kiraia katika masuala ya jinsia na Katiba nchini Tanzania Bi. Victoria Mandari.

Mwenyekiti wa muungano huo Bi. Victoria Mandari ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam ikiwa ni tamko la pamoja la muungano huo unaounda mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali hapa nchini.

Amesema kumekuwepo na shinikiza la kisiasa la kuwataka watanzania waikatae katiba hiyo pendekezi jambo ambalo linaweza kusababisha hata yale mazuri yaliyokuwepo ndani ya katiba hiyo yakaonekana ni mabaya.

Bi. Victoria amesema Katiba hiyo inayopendekezwa imebeba asilimia kubwa ya maslahi kwa wananchi tofauti na wanasiasa wanavyoichambua kwa kutaka masuala ya kiutawala zaidi.