Muonekano wa eneo lililotolewa
Serikali imekabidhi eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta arobaini ambalo limetolewa na wananchi wa kijiji cha Burugo wilayani Bukoba bure, bila fidia yoyote kwa serikali ya china kwaajili ya ujenzi wa chuo cha ufundi stadi veta kitakacho jengwa kwa gharama ya shilingi bilioni tatu.
Akiongea mara baada ya kukabidhi eneo hilo pamoja na ramani ya mchoro wa chuo kitakachojengwa katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Profesa Sifuni Ernesti Mchome amesema lengo na madhumuni ya kukabidhi eneo hilo na ramani kwa serikali ya china ni kutaka kuharakisha ujenzi wa chuo hicho kwaajili ya kukuza elimu ya ufundi satadi kwa vijana wanaomaliza masomo ya kidato cha nne na sita kwaajili ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Mapema akiongea mara baada ya kukabidhiwa eneo hilo mwakilishi mkuu wa balozi wa china nchini Tanzania katika masuala ya uchumi na biashara Lin Zhiyoung amesema serikali ya China na Tanzania zimekuwa sikishirikiana kwa kiasi kikubwa katika masuala ya elimu na imesaidia katika shule za msingi na kutoa mafunzo kwa wataalaumu mbalimbali ambao wamekuwa wakienda China na kujifunza ujuzi kutokana na kazi wanazo zifanya nchini kwao.
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Burugo wamesema ardhi hiyo wameitoa kwa moyo mmoja na kwamba kamwe hakutoweza kutokea mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.

