Saturday , 13th Jun , 2015

Waendesha baiskeli wapatao 30 kutoka Uingereza wameanza safari ya kilomita 406 kutoka hifadhi ya Mlima Kilimanjaro hadi Ngorongoro.

Waendesha baiskeli wapatao 30 kutoka Uingereza wameanza safari ya kilomita 406 kutoka hifadhi ya Mlima Kilimanjaro hadi hifadhi ya bonde la Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania, kwa ajili ya kukusanya takribani shilingi milioni 350 za Tanzania ili kusaidia mradi wa usalama barabarani na Afya hapa nchini.

Wakizungumza jijini Arusha wakiwa njiani kuelekea hifadhi ya bonde la Ngorongoro, mkuu wa msafara ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Michelin nchini Uingereza na Ireland, Guy Heywood amesema kuwa mpango huo wa mbio za hisani ni wa tatu na utakuwa ukifanyika kila mwaka.

Heywood amesema kuwa kampuni hiyo kupitia wakala wao Tanzania imekuwa ikilichangia shirika hilo kama sehemu ya mchango kwa jamii, ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watanzania kupitia mpango wake wa kupunguza ajali na kusambaza huduma za afya vijijini kwa takribani miaka 15 sasa