Monday , 28th Nov , 2016

Vijana wameiomba serikali kuweka mazingira wezeshi ili kuweza kuajiajiri, kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo baada ya kuhitimu elimu mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyuo vya ufundi wanavyosoma hapa nchini na kupunguza tatizo la ajira kwa kiasi kikubwa

Mkuu wa Chuo cha VETA Makete, Ramadhan Sebo akitoa nasaa kwa wanafunzi wanaoingia mtaani kujiajiri.

 

Vijana hao wamesema kuwa serikali iondoe vikwazo vidogovidogo katika kuanzisha miradi ili waweze kuanzisha miradi na kutoa mitaji kwa wanaohitaji kuanzisha miradi na kukwama katika mitaji.

Ombi hilo limetolewa wahitimu hao wa chuo cha Veta wilaya ya Makete mkoani Njombe katika Mahafali ya pili cha chuo hicho huku mabweni nayo yakitajwa kuwa kikwazo cha wengine kuendelea na masomo.

Mkuu wa chuo cha VETA Makete Ramadhan Sebo, anasema kuwa chuo hicho kimefikia mafanikio ya kupata vifaa vitakavyowawezesha vijana hao kuweza kujiajiri baada ya kuhitimu mafunzo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Makete Emmanuel Namaumbo amewataka vijana hao baada ya kumaliza masomo yao wajiunge katika vikundi na waanze kufanya kazi ili waweze kupata mgao katika zile milioni 50 kwa kila kijiji.