Wednesday , 22nd Jun , 2016

Serikali ya Tanzania imesema kuwa inatarajia kushuka kwa gharama za usafiri wa anga nchini baada ya serikali kuondoa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika usafiri wa anga.

Serikali ya Tanzania imesema kuwa inatarajia kushuka kwa gharama za usafiri wa anga nchini baada ya serikali kuondoa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika usafiri wa anga.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uchukuzi na Mawasilianao Mhe. Makame Mbarawa wakati akifungua mkutano wa kumi na tisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na Usafirishaji unaofanyika Jijini hapa kwa nchi za wanachama wa Jumuiya ya SADC.

Mkutano huo unaojumusha nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), lengo kuu likiwa ni kujadili usalama wa usafiri wa anga pamoja na changamoto nyingine za usafiri huo katika nchi hizo za
Akielezea hali ya usalama wa anga nchini katika mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya viwanja vya ndege na usafirishaji wa Tanzania Hamza Johari amesema kuwa ugaidi bado ni changamoto kubwa ambayo ni vyema mamlaka zikaendela kukubaliana namna ya kuondokana nao baada ya kuona dalili za kutumiwa viwanja vya ndege kwa vitendo hivyo.