Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Bahame Nyanduga
Akizungumza na East Africa Radio Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw, Bahame Nyanduga amesema wasimamizi hao wahakikishe kwamba zoezi hilo linaendeshwa kusimamia sheria za uchaguzi, na uwazi tangu mwanzo wa upigaji kura mpaka utoaji matokeo.
Nyanduga ameongeza uzeofu unaonesha katika nchi nyingine moja wapo kati ya hatua za uchaguzi zikivurugika zinaweza kuleta maafa na kutaka tume kuzingatia maadili na usawa kwa vyama vyote.
Katika hatua nyingine amewasifu wananchi wanaojitokeza katika mikutano ya kampeni kwa utulivu na amani wanayoionesha huku akisisitiza waendelee kuwa hivyo mpaka siku ya uchaguzi mkuu.
Aidha mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kuwapa pole wale wote waliohofiwa na ndugu zao katika moja ya mikutano ya kampeni ya CCM na waliojeruhiwa waweze kurejea katika hali yao ya kawaida huku akiongeza vyama vya siasa vinatakiwa kutafuta viwanja vilivyo na usalama wa kutoka na kuingia.