Mtalamu wa vifukofuko kuto Tanga Ladislaus Ng'ingo akitoa elimu jinsi ya kuhifahi mahindi.
Akizungumza na kituo hiki mwakilishi wa PPTL kutoka mkoani Tanga ambao ni wazalishaji wa mfuko wa tabaka tatu uitwao PICS, Ladislaus Ng'ingo amesema kutokana na ongezeko la upotevu wa mazao kabla na baada ya kuvuna mifuko hiyo itasaidia kuzuia wadudu kuingia.
Naye mshauri wa masuala ya kibiashara katika mradi huo Bernadeta Majebele ametoa wito kwa wakulima kutumia teknolojia hiyo ili iwasaidia kuhifadhi mazao kwa usalama wa chakula katika ngazi ya kaya.
Naye Francis Mwitumba ambaye ni mratibu wa mradi huo kutoka Shirika la Caritas na Maendeleo Jimbo Katoliki la Mbeya amesema mradi huo upo katika wilaya tano na vijiji 453 mkoani ambavyo vipo kwenye mpango huo.