Wednesday , 29th Jun , 2016

Tanzania inategemewa kuwa mwenyeji wa mkutano utakaowakutanisha wadau mbalimbali kutoka Afrika na Dunia kwa ujumla kwa lengo la kujadili jinsi ya kupambana na masuala ya uhalifu wa kimtandao.

Akiongea na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Idara ya TEHAMA Dkt. Shaaban Pazi amesema kuwa mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kesho utajadili jinsi ya kuimarisha usalama wa taarifa na data na kupunguza wizi wa kimtandao ambapo takwimu zinaonesha kiasi cha dola bilioni 300 hupotea duniani kote kutokana na wizi wa kimtandao.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya Oracle Corporation for Race Region Bw. Janusz Naklick amesema kuwa wameamua kuandaa mkutano huo nchini Tanzania sababu nchi ya Tanzania inaonekana kupiga hatua katika masuala ya mawasiliano.