
Mkuu Mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi.
Hayo yamezungumzwa na mkuu Mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya huduma jumuishi kuzuia maambukizi ya UKIMWI kitaifa yanayofanyika mkoani humo.
Dkt. Nchimbi amesema ili kufanikiwa kudhibiti maambukizi mapya ya VVU taasisi za kisheria ni lazima kushughulika na watuhumiwa wa vitendo vya ubakaji na ulawiti.
Uzinduzi huo uliobebwa na kaulimbiu ya 'Kuwa mjanja afya ndiyo dili', upimaji wa maambukizi UKIMWI, na magonjwa ya salatani, tezi dume pamoja na huduma zingine za uzazi wa mpango,tohara na uchangiaji wa damu zinatolewa.
Kampeni hii itatekelezwa katika mikoa 10 ambayo maambukizi yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na Katavi, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Rukwa, Shinyanga, Pwani, Tabora, Dar es Salaam lengo likiwa ni kuhimiza jamii juu ya mapambano dhidi ya UKIMWI