Mwenyekiti wa Baraza la watoto la wilaya ya Arusha, Dominic Raphael
Hayo yameelezwa katika Baraza la watoto la wilaya ya Arusha lilokutana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo haki za watoto ,Mjumbe wa Baraza hilo Hassan Kimaro amesema kuwa ili kuwa na taifa bora lenye ustawi ni vyema kukemea vitendo vya kikatili kwa watoto ili visigeuke desturi na kuathiri maendeleo ya taifa
Mwenyekiti wa Baraza hilo Dominic Raphael na Mjumbe wa Baraza hilo Brina Salvatory, amesema kuwa kwa sasa wamejikita katika kutetea haki za hususan wale wanaofichwa majumbani na kuhakikisha kuwa wanafichuliwa ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu na mlo bora
Mratibu wa wanawake na watoto jiji la Arusha ,Saumu Kweka amesema kuwa Baraza hilo la watoto limesaidia kufichua vitendo vya kikatili dhidi ya watoto na kuziwezesha mamlaka husika kuchukua hatua kali.
Changamoto inayowabili watoto nchini ni pamoja na matukio ya kikatili wanayofanyiwa majumbani ambayo asilmia kubwa hayaripotiwi katika vyombo vya sheria ,suala linalofanya ukatili wa kijinsia kukosa mwarobaini wa kisheria ambao unaweza kukomesha vitendo hivyo.