Monday , 28th Nov , 2016

Serikali imeombwa kuboresha miundombinu ya barabara na vituo vya afya wilayani Arumeru kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua kwa kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma katika vituo vya afya maeneo ya vijijini.

Mkuu wa Makosa ya Jinai Wilayani Arumeru John Mwakaluka.

 

Hayo yameelezwa na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya usalama barabarani yanayoendeshwa na shirika la (APEC) ambapo Bi Debora Laizer ameeleza kuwa akina mama wengi wamekuwa wakihatarisha afya zao kwa kuchelewa kupata huduma za afya kwani barabara ni changamoto ili kufika kituo cha afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Makosa ya Jinai Wilayani Arumeru John Mwakaluka ametumia fursa hiyo kuwaasa wahitimu hao hususani madereva wa bodaboda kujenga tabia ya kufahamiana katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kudhibiti matukio ya kiuhalifu nchini.

Sanjari na hayo Mkurugenzi wa (APEC) Respicious Timanywa naye akahitimisha kwa kutoa rai kwa jamii ya wamasai kuvunja mila potofu na kuhakikisha watoto wa kike wanapelekwa shuleni na si kuozeshwa wakiwa na umri mdogo kwa ajili ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.