Monday , 25th Jul , 2016

Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imeanza mradi wa uboreshaji wa Makazi Jijini Mbeya kupitia Program ya urasimishaji wa makazi ambayo inafanywa kwa majaribio.

Moja ya Mitaa inayopatikana Mbalizi Jijini Mbeya.

Mratibu wa mradi wa kuboresha Makazi wa Mkoa wa Mbeya Enock Kyando,amesema utekelaji wa mradi huo utekelezaji wa mradi huo utakuwa ni wa miezi 6 ambao unakwenda na utoaji wa hati miliki za viwanja kwa gharama nafuu na kuondoa ujenzi holela.

Kyando amesema kuwa kati ya faida ambazo zinapatikana kutokana na mradi huo ni pamoja na serikali kukusanya mapato ya kodi kutoka maeneo hayo jambo litakalosaidia kukuza uchumi wa nchi, lakini pia na wananchi kumiliki viwanja vyao kihalali kwa kukabidhiwa hati miliki.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika amesema kuwa kutoka na Ardhi ya sasa kuwa na thamani ndio maana ukaanzishwa mradi wa urasimishaji unapelekwa katika maeneo ambayo yamejengwa kiholela ambapo kwa Mbeya umeanzia eneo la Mbarizi.

Mradi huo wa majaribio wa kuboresha Makazi unatekelezwa kwa mikoa mitatu nchini ambayo ni ,Morogoro, Tabora na Mbeya huku wananchi wakisifu mpango huo kwa kuwa na imani unaweza kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Sauti ya Mratibu wa mradi wa kuboresha Makazi wa Mkoa wa Mbeya, Enock Kyando.