Friday , 23rd May , 2014

Serikali ya Tanzania imeanza kupanua mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu juu ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 82 hadi lita milioni 196 kwa siku, ili kukabiliana na uhaba wa maji kwa wakazi wa mikoa ya Pwani na jiji la Dar es salaam.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini Tanzania, Profesa Jumanne Maghembe.

Akitoa taarifa ya tatizo la upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam, leo Bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe amesema serikali imeingia mkataba wa ujenzi huo ambao utakamilika Desemba mwakani na wakandarasi wawili kutoka nchini India ili kuongeza kiwango cha upatikananji wa maji safi na salama kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Aidha, Prof. Maghembe amesema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na wezi wa maji jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa wizi na waliobainika kutenda kosa wametozwa faini na wengine kufungwa.