
Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu wa Baraza la ujenzi nchini Bwana Ipyana Moses amesema asilimia kubwa ya majengo nchini yanatumia garama kubwa katika uendeshwaji hasa wa umeme kutokana na ujenzi wa kizamani ambao si rafiki kwa mazingira.
Ipyana amesema, endapo wajenzi watatumia ujuzi wao kubuni na kujenga majengo ya kisasa itawasaidia wapangaji na watuaji wa majengo hayo kupata manufaa makubwa ya kiafya na kimazingira.
Naye mtaalamu wa miundombinu ya kiuandisi katika nyumba Eng. Menye Manga amesema, asilimia 80 ya magorofa jijini Dar es salaam nivyema yakabadilishwa ili kulinda taifa na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi kwani majengo hayo yanatumia nishati nyingi sana.