Monday , 28th Nov , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe ameondoa zuio la kilimo cha mahindi mkoani Singida liliwekwa miaka kadhaa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo kwenye serikali ya awamu ya nne.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe.

 

Zuio hilo lilipiga marufuku kilimo cha mahindi mkoani humo pamoja na kuliondoa zao hilo kwenye orodha ya mazao yanaoyozalishwa na mkoa huo kwa madai kuwa haliwezi kustahimili mvua chache inayonyesha nmkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida amesema ametengua zuio hilo mara baada ya kufanyika utafiti wa uzalishaji wa mahindi kwa watu waliokaidi agizo hilo na kuona kuwa kwa sasa wakulima wanaweza kuanza rasmi uzalishaji wa zao hilo.

Mitigumwe amesema kuwa licha ya kuruhusiwa kwa kilimo hicho na tayari kwa ajili ya kupokea pembejeo za kilo kwa zao hilo lakini wakulima watapaswa kulima mazao yanayohimili ukame ndipo wazalishe mahindi kama zao la chakula.