
Sehemu ya banio la kukingia maji kwenye chanzo cha maji (chemchem) katika kijiji cha Malonje.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe, mhadisi wa mkoa, Christopher Nyambiga amesema kuwa serikali katika ujenzi wa chanzo cha maji cha Nyenga imeokoa jumla ya shilini milioni 350 ambazo serikali kama ingeweka msimamizi katika mradi huo angezihitaji fedha hizo na kuukamilisha mradi huo.
Nyambiga ameyasema hayo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara ya Naibu Waziri wa Maji ya siku mbili mkoani humo na kutembelea katika vyanzo mbalimbali vya maji mkoani humo ambavyo vinaendelea kuboreshwa na vile vipya ambavyo vinajengwa katika mkoa wa Njombe.
Amesema kuwa ofisi yake ilichukua jukumu la kuusimamia mradi huo ili kuokoa pesa za usimamizi kwani kulikuwa na wataalam katika ofisi hiyo wenye uwezo wa kusimamia mradi huo na wana taaluma kama ya mtu yeyote ambaye angepewa mradi huo.
Amesema kuwa mradi huo umekamilika na umeenda vizuri na kuwa mwezi Machi mradi huo unaanza kufanya kazi na maji yatakuwa yameongezeka kutoka asilimia 43 mpaka asilimia 79 na kupunguza tatizo la maji mkoani Njombe.
Nyambiga ametoa ushauri kwa wakandalasi mbalimbali walioajiriwa na serikali kuhakikisha kuwa wanaokoa pesa kama walivyofanya wao na kuwa kama kuna kazi wanaiweza waisimamie wao wenyewe na kuachana na kuweka msimamizi ambaye angehitaji fedha nyingi katika mradi mmoja.
Mradi huo ni moja ya miradi ambayo Naibu Waziri wa Maji Amos Makalla, maeipitia katika ziara yake ya siku mbili mkoani Njombe na kusifia kazi iliyofanyika na kuwa ni moja kati ya miradi iliyojengwa kwa ustadi wa hali ya juu.