Saturday , 13th Jun , 2015

MKOA wa Njombe umeiomba taasisi inayo husika na utoaji wa takwimu za maambikizi ya UKIMWI na mwenendo wake hapa nchini kwa lengo la kujipima mapambano yao kama yamefanya kazi ama hayajafanya kazi.

Sehemu ya mkoa wa Njombe

Ombi hilo limetolewa na katibu tawala mkoa wa Njombe Jackson Saitabahu wakati wa mkutano wa wadau wa kupambana na maambukizi ya UKIMWI mkoa wa Njombe kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa mapambano ya UKIMWI mkoani huo ulio shirikisha mashirika yasiyo ya serikali na wawakilishi wa wafadhiri.

Akifungua mkutano huo Saitabahu amesema kuwa asingependa kusikia mkoa wa Njombe kuwa unaongoza kwa asilimia 14.8 kitaifa kwa maambukizi na kuwa anaomba Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS kufanya utafiti wa maambukizi ya UKIMWI ili kutoa takwimu mpya.

Amesema kuwa wadau mkoa wa Njombe wamekuwa wakipambana kila kukicha jinsi ya kushusha maambukizi ya UKIMWI na kuna uhakika wa kushuka kwa maambukizi na lengo ni kufikia sifuri tatu ambapo maambukuzi mapya sifuri, Unyanyapaa sifuri na vifo vitokanavyo na Ukimwi sifuri.

Aidha mratibu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, mkoa wa Njombe Abubakari Magege, amesema kuwa mwaka ujao kuna mpango wa kuanza kufanya utafiti wa maambukizi ya UKIMWI na Malaria nchi nzima na kuwa takwimu mpya ndipo zitatolewa.