
Mfanyabishara Mohammed Dewji.
Kupitia mtandao wake wa 'twitter' Mo Dewji ameandika kuwa, "Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu".
Mo Dewji ameongeza kuwa, "Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima".
Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu. Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima.
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) October 22, 2018
Mfanyabishara huyo alitekwa na watu wasiojulikana Alfajiri ya Oktoba 11, wakati akielekea mazoezini na kuachiwa Alfajiri ya Oktoba 19, ambapo alikutwa ametelekezwa katika viwanja vya Gymkana.