Monday , 11th Jan , 2016

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) wilaya ya Geita Bwana Mhere Mwita, amewatetea wachimbaji wadogo katika wilaya hiyo kuwa wana haki ya kupewa kuchimba dhahabu ili kuepuka kuuliwa na Askari mgodi.

Bwana Mhere Mwita amesema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Magufuli inatakiwa kuwaangalia wachimbaji wadogo wadogo wilaya Geita kwa huruma na itatue kero hiyo.

" Wachimbaji wadogo hapa wilayani wapewe sehemu ya kujichimbia dhahabu ili kuondokana na Vifo vya vijana ambao huwa wanauwawa kila siku na Askari wa Mgodi wa Geita wanapoenda kuchukua mabaki ya mawe yaliyotupwa alimaarufu kwa jina la (Magwangara)". Amesema Mwenyekiti huyo wa BAVICHA Bwana Mhere

Mhere amesema mateso kwa wananchi hao wa Geita sasa yafikie mwisho kwani kila mwananchi ana haki katika nchi yake na serikali isikie kilio cha wachimbaji hao