Wednesday , 9th Apr , 2014

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Julius Mtatiro ameonyesha hofu yake juu ya uwezekano wa mchakato wa kupata Katiba mpya ya Tanzania kukamilika kwa wakati kutokana na kukabilwa na changamoto nyingi.

Mjumbe wa bunge maalumu la katiba na naibu katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF (Tanzania Bara) Julius Mtatiro

Akizungumza leo na East Africa Radio, Bw. Mtatiro ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Upinzani cha (CUF) Tanzania Bara, amesema hali hiyo inachangiwa na Chama Tawala cha CCM kuhodhi mchakato mzima wa Katiba.

Mtatiro amefafanua hali hiyo imechangia matukio ya mara kwa mara ya kuvurugika kwa mchakato huo hasa baada ya wajumbe kutoka makundi mengine yenye uwakilishi katika bunge hilo kuona kuwa hayatendewi haki na wenzao wa CCM ambao amedai kuwa wamehodhi mchakato huo.