Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mkuu wa Mkoa Pwani atoa maagizo

Monday , 25th Sep , 2017

Viogozi wa vijijiji na mitaa wametakiwa kutoa ushirikiano kwa wadadisi wa utafiti wa kilimo ili serikali iweze kupata  taarifa sahihi ya maendeleo ya wakulima .

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo katika Mafunzo ya wadadisi wa utafiti wa kilimo wa mwaka 2016/17 yaliyofanyika mjini Kibaha.

"Nawaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi na wasimamizi wa takwimu, kwa kutoa taarifa sahihi kuhusiana na utafiti huu , napenda niwahakikishie wananchi kuwa kwa mujibu wa sheria ya takwimu namba tisa ya mwaka 2015, taarifa zitakazokusanywa zitatunzwa kwa usiri na zitatumika kwa shughuli za kitakwimu tu", alisema.

Ndikilo alisema sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi ambapo kwa mwaka 2016 ilichangia pato la taifa kwa asilimia 29.1 ,  na kati asilimia hiyo kilimo cha mazao kilichangia asilimia 15.5, mifugo, 7.7, misitu 3.9 na sekta ya uvuvi ilichangia asilimia 2.0.

"Sekta ya kilimo inaajiri  zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania wote wenye uwezo wa kufanya kazi hasa katika maeneo ya vijijini, kwa hivyo mafunzo haya ya leo ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mipango ya kuboresha maisha ya watanzania walio wengi," alisema .

Hata hivyo Ndikilo alitoa agizo kwa watumishi hao kujifunza kwa bidii mafunzo hayo ya siku tano na kuwa watakaofaulu ndio watakwenda kufanya shughuli hiyo ya ukusanyaji wa data vijijini.

Naye mratibu wa mafunzo hayo kanda ya mashariki ,  mtakwimu kutoka makao makuu, Theresia Sagamilwa alisema mafunzo hayo yatawasaidia wadadisi kupata taarifa sahihi za kilimo ili kuisaidia serikali ijue maendeleo ya wakulima na mahitaji yao halisi ili kujua namna ya kuwasaidia.

 

 

HABARI ZAIDI

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani