Tuesday , 26th Jul , 2016

Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA), imesema itamfikisa mahakamani mtendaji mkuu wa mabasi yaendayo haraka (UDA-RT),David Mgwasa kwa kupandisha nauli.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT), Bw. David Mgwassa

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra Gilliard Ngewe, na kuongeza kuwa utaratibu wa watoa huduma wa mabasi hayo kuongeza nauli kwa mabasi yanayoanzia Mbezi kuptia njia kuu kufikia shilingi 1050 badaya la 800 hautakubalika.

Ngewe amesema kuwa wameshapeleka barua kadhaaa za onyo kwa mtendaji huyo lakini bado wameendelea kupokea malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma hizo kuhusu kuendelea kwa hali hiyo.

Mkurugenzi huyo wa Sumatra amesema mashtaka kwa ajili ya Mkurugenzi wa UDA-RT tayari yameshaandaliwa na kwamba muda wowote atafikishwa mahakamani kuyajibu.