Monday , 11th Apr , 2016

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Khamisi Kigwangala, ameupa uongozi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Manyara, muda wa mwezi mmoja kutatatua changamoto za uhaba wa damu katika mkoa huo.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Khamisi Kigwangala

Dkt. Kigwangala amesema hayo baada ya kutembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara, iliyopo mjini Babati na kushuhudia hospitali hiyo ikiwa haina damu ya kutosha kwenye benki yake.

Naibu Waziri huyo amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Ally Uledi, kuanisha mipango ya upatikani wa damu salama katika kipindi cha siku 30,baada ya kushuhudia benki ya damu ikiwa na unit 3 badala ya 150 zinazohitajika.

Aidha, Dkt. Kigwangala ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa kuwa na chumba maalumu cha kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum ambapo amesema wajenge walau vyumba viwili kwa ajili ya shughuli hiyo.

Dkt. Kigwangala amesema kuwa kutokana na hospitali kuhudimia idadi kubwa ya watu haiwezi kufanya kazi ikiwa haina damu ya kutosha vitanda vya kutosha na hata chumba maalum cha wagonja wanaohitaji uangilizi maalum hivyo mkoa huo hauna budi kufanya juu chini kuweza kutatua changamoto hiyo.

Sauti ya Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Khamisi Kigwangala.