Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Majaliwa afurahishwa na maendeleo

Tuesday , 12th Sep , 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiri kufurahishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.

Furaha ya Bw. Pardesi  imekuja mapema leo  Septemba 12,baada ya kukutana na Waziri Mkuu kwenye  makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam ambato Mh. Waziri Mkuu amesema kwamba tayari Serikali imeanza kuwahamasiha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

Waziri Mkuu amempongeza Bw. Pardesi kwa kuiunga mkono Serikali katika mpango wake wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda. Kampuni ya Namera Group of Industries inamiliki kiwanda cha nguo cha NIDA na cha Namera vya jijini Dar es Salaam.Kampuni inatarajia kufungua kiwanda kingine cha nguo wilayani Kahama.

Pia Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha zao la pamba linapewa kipaumbe alikutana na wakuu wa mikoa yote inayolima pamba Ijumaa, Septemba 8, 2017 na aliwaagiza wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi hususan wakulima wa zao la pamba.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kusimamia kilimo cha pamba kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko, hivyo ahadi yao ya kununua pamba yote ni faraja kwa wakulima.

"Nimefurahishwa na uamuzi wenu wa kutaka kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao kwani kwetu sisi ni faraja kwa sababu wakulima walipunguza uzalishaji baada ya kukosa soko la uhakika," amesema

Upande wake Bw. Pardesi amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba kampuni yao inauwezo wa kununua pamba yote inayozalishwa nchini na kuichakata katika viwanda vyao na kutengeneza nguo zitakazouzwa nchini kwa bei nafuu.

Amesema kwa sasa wameajiri mafundi katika viwanda vyao ambao watakuwa wa nashona nguo na kuziuza nchini kwa gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kumudu kununua na kuondokana matumizi ya nguo za mitumba.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi Namera tuko tayari kununua pamba yote inayozalishwa nchini kwani viwanda vyetu vinafanya kazi ya kuchambua pamba, kutengeneza nyuzi na majora kisha tunashona nguo na kuziuza. Hapa Kazi Tu maana bila ya kufanya kazi huwezi kuheshimika."  Bw. Pardesi.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kitendo cha kununua pamba inayolimwa nchini na kuchakata katika viwanda vyao kwa lengo la kutengeneza nguo za aina mbalimbali wataiwezesha Serikali kuokoa fedha nyingi za kigeni zilizokuwa zinatumika kuagiza nguo nje ya nchi.

HABARI ZAIDI

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba