Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Majaji wapewa angalizo mitandao ya kijamii

Tuesday , 19th Sep , 2017

Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, ametoa angalizo kwa Majaji wafawidhi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii katika mahusiano pamoja na kutoa michango kwenye mitandao hiyo juu ya jumbe zisizofaa.

Jaji Mkuu ametoa  angalizo hilo wakati akifunga mkutano wa Majaji wafawidhi wa kanda nchini, uliofanyika Jijini Arusha 

"Katika suala la matumizi ya mitandao, kuweni makini. Msi- like picha ambazo hazina maadili au kuchangia kwa kutoa maoni katika mitandao ya kijamii," alisema.

Aidha, amewataka kuwa makini na ndugu au jamaa wanaowatembelea, akisema baadhi yao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali ya kijinai.

Aliwataka majaji hao kujenga tabia ya kupenda kujisomea na kuelewa mabadiliko yanayofanywa na Bunge kwa kurekebisha sheria ili kuweza kugundua makosa mbalimbali yanayofanywa na Mahakama za chini na wafundishane namna ya kuboresha hukumu zinazotolewa ili kupunguza mrundikano wa mashauri.

"Ni vizuri kuelewa mabadiliko yanayofanywa na Bunge wakati wa kurekebisha sheria, kazi na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa katika kufungua mashauri," alisema.

Kuhusu migongano kati yao na vyombo vingine vya serikali, aliwataka kutambua mipaka ya vyombo hivyo na wao watambue mipaka yao huku akisisitiza kwamba kila chombo kikitambua mipaka yake wataheshimiana na hakutakuwa na mgongano katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mkutano huo wa majaji wafawidhi ulikuwa mahususi kutathmini na kuweka mikakati ya kumaliza mrundikano wa mashauri 2,198 yaliyopo Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, kati yao mengine yamekaa zaidi ya miaka 10.
 

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao