Monday , 6th Oct , 2014

Serikali nchini Tanzania imesema imeongeza juhudi katika kutatua changamoto zinazoikumba sekta ya elimu hasa maslahi ya walimu na kusema kwa sasa wanalishughulikia suala la kumaliza madeni yao.

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungao wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Akiongea Katika maadhimisho ya siku ya Walimu ambayo kitaifa yalifanyikia wilayani Bukoba Mkoani Kagera Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungao wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amesema kwa kutambua umuhimu wa kada ya Ualimu serikali itahakikisha inafanya jitihada za kulipa madai yao pamoja na kuwaandalia mazingira mazuri ya kuishi na kufundisha.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Jenister Mhagama amesema kwa sasa wametoa fursa nyingi zaidi kwa walimu ikiwemo kujiendeleza kitaaluma.

Wakati huo huo, baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Monduli Jijini Arusha nchini Tanzania wamalalamikia migogoro ya ardhi inayoendelea kuyakabili maeneo ya wafugaji na wakulima na kusema kuwa inavyoonesha migogoro hiyo ina maslahi kwa viongozi ndio maana wanaifumbia macho.

Akizungumzia malalamiko hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Bw. Edward Sapunyo amesema tatizo lipo zaidi kwa viongozi wa kata na vijiji na kunachangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa migogoro hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Monduli Bw. Twalibu Mbasha amesema pia Halmashauri inaendelea kukabiliana na tatizo kubwa la baadhi ya watu wenye uwezo mkubwa kifedha kutumia umasikini na uelewa mdogo wa sheria unaowakabili wananchi kupandikiza migogoro.