
Naibu waziri wa fedha na uchumi nchini Tanzania, Adam Kigoma Ali Malima.
Mhe. Malima ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na wananchama wa chama cha waandishi wa habari za kodi nchini Tanzania TAWNET kwa lengo la kutoa msisitizo kwa chama hicho
katika utoaji wa elimu kwa wananchi kuelewa umuhimu wa ulipaji kodi.
Mhe Malima akizungumzia suala bajeti kwa mwaka wa fedha 2014/2015 amesema kipaumbele kimeelekezwa zaidi katika maboresho kwenye sekta ya kilimo, afya na elimu ili kuleta maendeleo ya kiuchumi.