Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kikwete 'alivyopora dili' la kiwanda cha vigae

Sunday , 19th Feb , 2017

Ujanja, na uwezo mkubwa wa kujiongeza kwa Mbunge wa Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete ndiyo mambo yaliyosababisha kiwanda kipya cha vigae kijengwe Chalinze badala ya Mkuranga mkoani Pwani kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiambatana na Waziri Charles Mwijage kukagua eneo ambapo kitajengwa kiwanda cha vigae.

Kikwete akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast amesema aliweza kujenga hoja kwa wawekezaji waliokuja nchini kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho, zilizotosha kuwashawishi ni kwanini wajenge Chalinze badala ya Mkuranga.

Miongoni mwa hoja alizojenga ni pamoja na jiografia ya eneo la Chalinze kuwa kitovu cha mikoa karibu yote ya Tanzania kwa kuwa ni njia panda, na pia Chalinze kuwa ni kitovu cha kibiashara kwa kuwa kuna urahisi wa usafirishaji wa bidhaa hiyo kwenda mikoa mbalimbali na hata nje ya nchi.

Pia amesema Chalinze ni eneo ambapo kuna urahisi wa kupata malighafi kwa ajili ya utengezaji wa bidhaa hiyo, ambapo Chalinze ni katikati ya maeneo yote ambako malighafi hizo zinaweza kupatikana ikiwa ni pamoja na Pugu, Rufiji, Iringa na Morogoro.

"Hawa watu wa Tryphod walipokuja, kwanza walitaka kuwekeza Mkuranga, nikapata fursa ya kwenda kuonana na Meneja Rasilimali Watu wao, nikazungumza nao, na nikamueleza kuwa fursa kubwa za kibishara ziko Chalinze". Amesema Kikwete

Amesema baada ya kuwashawishi, walimuelewa na kukubaliana naye, huku akiungwa mkono pia na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

Ametaja miongoni mwa manufaa yatakayopatina ni pamoja na fursa ya ajira kati ya 6000 hadi 8000 kwa wakazi wa eneo hilo na nje ya eneo hilo, na tayari ujenzi umekwishaanza.

Msikilize hapa akiwa kwenye mahojiano na Shaaban Lupa wa EA Breakfast.

 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya