Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Hii ni historia kwa Tanzania

Thursday , 19th Oct , 2017

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Barick nchini imekubali kulipa fidia ya dola milioni 300 ambazo sawa na bilioni 700 za Tanzania, pamoja na kuweka mgao sawa wa faida wa 50/50 na serikali, kufuatia mazungumzo ya ripoti ya makinikia yaliyofanyika.

Rais Magufuli akiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya migodi ya dhahabu ya Barrick, John L. Thornton

Taarifa hiyo ambayo ni mara ya kwanza kutokea kwenye historia ya Tanzania, imetolewa leo na serikali wakati ikikabidhi ripoti ya mazungumzo hayo kwa Rais John Pombe Magufuli, na kusema kwamba licha ya makubaliano hayo, pia kampuni hiyo imekubali masharti yote yaliyowekwa kufuatia mazungumzo hayo, ili nchi iweze kunufaika na rasilimali zake.

Pia kwenye ripoti hiyo imekubaliwa kuwa migodi yote itaweka fedha zake kwenye akaunti zilizopo hapa nchini, na serikali kubakia na umiliki wa madini yote yatakayokuwepo kwenye makinikia, ukiondoa dhahabu, shaba na fedha ambayo yatakuwa yanamilikiwa na Barrick kisheria.

Pamoja na hayo makubaliano yaliyofikiwa yameitaka kampuni hiyo kuwapa ajira za kudumu wazawa wa eneo husika, na kuwapa stahiki zote kama wafanyakazi, na wamekubali kulipa kile kinachostahili kwenye halmashauri husika ambako migodi ipo.

Kufuatia ripoti hiyo Rais Magufuli ameipongeza timu iliyohusika kwenye mazungumzo hayo, na kuwataka Watanzania kushirikiana katika kuleta maendeleo ya nchi.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea