Tuesday , 25th Nov , 2014

Kufuatia kuwepo kwa Taarifa za suala kujadiliwa kwa ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow kupelekwa mahakamani ili usijadiliwe na Bunge la Jam, Spika wa Bunge Bi. Anna Makinda amesema hakuna Muhimili utakaoweza kuingilia Shughuli za bunge.

Kufuatia kuwepo kwa Taarifa za suala kujadiliwa kwa ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow kupelekwa mahakamani ili usijadiliwe na Bunge, Spika wa Bunge Bi. Anna Makinda amesema hakuna Muhimili utakaoweza kuingilia shughuli za bunge.

Akitoa Muongozo wake Baada ya Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. John Cheyo kutaka kujua ni hatua gani zitachukuliwa na Bunge dhidi ya suala hilo kufikishwa mahakamani Spika Makinda amesema kinga za Bunge ziko wazi na hakuna mtu anayeweza kuwashtaki ili wasifanye kazi yao.

Tamko hilo limetolewa na Spika Makinda baada ya maafisa wanao jitambulisha kuiwakilisha PAP kwenda mahakama kuu ya DSM kufungua shauri la kuzuia suala la Escrow kujadiliwa na Bunge.

Maafisa hao wa PAP wamefungua shauri namba 50 ya 2014 mahakama kuu kanda ya DSM ambapo wanamshitaki Waziri Mkuu, Spika, CAG na Katibu wa Bunge.

Hoja za PAP dhidi ya watu hao wanaoshitakiwa ni kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati, kudai faida ya mahakama kwa jambo lililokwisha kutolewa hukumu pia wanadai kukaguliwa na CAG na kuzuia mjadala wowote wa suala hilo hadi ufafanuzi wa mahakama utakapo tolewa.

Aidha Spika Makinda ameongeza kuwa leo mchana wataweza kuigawa ripoti ya CAG kwa wabunge ili kuweza kuisoma kwa kina ili waweze kuijadili taarifa ya kamati ya PAC, ambayo bado hajapewa taarifa ya kukamilika kwake.

Tags: